Mahakama Yazuia Kikao cha Bunge

Mahakama Yazuia Kikao cha Bunge

Mahakama ya Katiba Nchini Hispania, imezua kikao cha Bunge la Jimbo la Catalonia kilichopangwa kufanyika Jumatatu kuamua suala la uhuru wa jimbo hilo.

Mahakama hiyo imesema, hatua hiyo ni sawa na uvunjaji wa Katiba ambapo uamuzi huo umetokana na pingamizi lililowasilishwa na chama cha Kisoshalisti cha Catalonia ambacho kinapinga jimbo hilo kujitenga.

Mapema Waziri Mkuu wa Hispania, Mariano Rajoy, aliionya serikali ya Catalonia dhidi ya kujitangazia uhuru baada ya kura iliyopigwa Jumapili iliyopita kuamua hatma ya jimbo hilo.
Kiongozi wa Catalonia, Carles Puigdemont alidokeza kwamba, tangazo la uhuru wa jimbo hilo lingetolewa wiki ijayo katika kikao maalum cha Bunge.

Continue reading here: 

Mahakama Yazuia Kikao cha Bunge