Mahakama yamfutia kesi Manji

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopo jijini Dar es salaam imemfutia mashtaka yaliyokuwa yakimkabiri mfanyabiashara, Yusuph Manji ya matumizi ya dawa za kulevya.

Mashtaka hayo yamefutwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha mara baada ya upande wa mashtaka na wa utetezi kufunga ushahidi huo ambao ulikuwa umepelekwa mahakamani.
Aidha, Sababu iliyopelekea kufutwa kwa kesi hiyo imetajwa kuwa ni upande wa mashtaka ambao ni serikali kushindwa kuthibitisha kosa la mfanyabiashara kama ilivyotarajiwa katika kesi hiyo, Manji anadaiwa kati ya Februari 6 na 9, eneo la Sea View, Upanga wilayani Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroine.
Mahakama imemuachia huru mfanyabiashara huyo ikiwa ni siku chache tangu shauri lake jingine la uhujumu uchumi liondolewe Mahakani hapo na Mkurugenzi wa mashitaka (DPP) ambaye alieleza kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Hata hivyo, Manji amewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga ambapo alijiuzulu wadhifa huo mapema mwaka huu, pia alikuwa Diwani wa Kata ya Mbagala kabla ya kuvuliwa nafasi hiyo baada ya kupoteza sifa

The post Mahakama yamfutia kesi Manji appeared first on The Choice.

Continue reading here:

Mahakama yamfutia kesi Manji