Imamu Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 30 Jela kwa Kosa la Kulawiti

Imamu Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 30 Jela kwa Kosa la Kulawiti

Mkazi wa Gongo la Mboto, Dar es Salaam, Imamu Hassan (37) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumlawiti mtoto wa miaka 13.

Hassan amehukumiwa kifungo hicho katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Rita Tarimo, wakati wa shauri hilo lilipoitishwa kwa ajili ya hukumu.

Hakimu Rita amesema wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo upande wa mashitaka ulipeleka mashahidi watano ambao wamethibitisha shitaka pasi kuacha shaka.

Akipitia baadhi ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, Hakimu Rita amesema mtoto huyo alikuwa anafanyiwa vitendo hivyo mara kwa mara na baadae kumpa sh. 2,000 huku akimuamuru asidhubutu kumwambia mtu yoyote.

More here:  

Imamu Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 30 Jela kwa Kosa la Kulawiti