Bulaya: Ninafuatiliwa na watu waliovaa mavazi ya kininja

Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA), Ester Amos Bulaya, amesema kuwa yupo katika hatari kubwa kutokana na kufuatiliwa na watu waliovalia mavazi ya kininja nyumbani kwake wilayani Bunda.

Bulaya ametoa taarifa hiyo alipokuwa akiongea na mwandishi wa East Africa Television, na kusema kwamba watu hao walimfuata nyumbani kwake wakiwa na gari aina ya Noah huku wamevaa kininja.
Aidha, amesema kuwa kwa bahati nzuri wakati watu hao wakienda kwake hakuwepo nyumbani, hivyo ndugu zake wakampigia simu ili asirudi nyumbani siku hiyo aweze kuokoa usalama wake..
Hata hivyo, ameongeza kuwa watu hao waliokuwa wakimtafuta walizunguka kwa baadhi ya ndugu zake akiwemo bibi yake na kumkosa, lakini alienda kutoa taarifa polisi na mkuu wa kituo kuanza kufuatilia suala hilo, lakini haikuchukua muda akahamishwa kituo cha kazi.

The post Bulaya: Ninafuatiliwa na watu waliovaa mavazi ya kininja appeared first on The Choice.

See the article here:  

Bulaya: Ninafuatiliwa na watu waliovaa mavazi ya kininja