Breaking News: Kiwanda cha Super Doll Chateketea kwa Moto

Kiwanda cha Super Doll Chateketea kwa Moto

Moto mkubwa umeteketeza kiwanda cha Super doll kilichopo barabara ya Nyerere Dar es Salaam mchana wa leo, na kuteketeza mali za kiwanda hicho.

Akiongea na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Kamanda wa polisi mkoa wa Temeke, Gilles Muroto, amesema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, na jeshi la zimamoto linafanya jitihada za kuzima moto huo.
“Ni kweli tuko hapa jeshi la zimamoto linaendelea kuzima moto likishirikiana na jeshi la polisi, na mpaka sasa bado hatujajua chanzo cha moto huu”, amesema Kamanda Muroto.
Katika tukio hilo la kuzima moto huo kulijitokeza changamoto kubwa ya magari ya kuzima moto, ambapo kati ya magari 10 ya zimamoto moja ndilo lenye uwezo wa kuzima moto katika kiwanda hicho.

More: 

Breaking News: Kiwanda cha Super Doll Chateketea kwa Moto