Video: Nimeingia TAKUKURU kijasusi nimetoka kijasusi – Joshua Nassari

Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari Jumatano hii aliwasili katika Makao makuu ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Jijini Dsm, kwaajili ya kuwasilisha ushahidi wa awamu ya pili wa tuhuma zinazo wahusu madiwani wanane waliohama CHADEMA na kujiunga na CCM katika baadhi ya kata Mkoani Arusha.

Mbunge huyo aliwasili Ofisini hapo majira ya Saa Nane kasoro mchana, nakuruhusiwa kutoka majira ya Saa kumi na moja jioni ambapo mbali na kutoa ushahidi huo pia amefungua jarada la kesi zinazowahusu madiwani hao kama alivyoagizwa na mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola.

Akiwa anaingia ofisini hapo Mbunge Nasari alionekana akiwa ameshika ‘Flash’ na ‘Hard Disk’ ambavyo pia amedai vifaa hivyo alibebea ushahidi wa kutosha

Hata hivyo mbunge huyo amedai kuwa usalama wa maisha yake uko mashakani kulingana na jumbe za vitisho anazopokea baada ya kufichua sakata hilo

VIDEO:

Visit site:  

Video: Nimeingia TAKUKURU kijasusi nimetoka kijasusi – Joshua Nassari