Timu ya Simba Kiboko…Mwendo wa Ushindi tu

Klabu ya soka ya Simba imeibuka na ushindi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Dodoma FC uliopigwa leo jioni kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Kikosi hicho ambacho kinajiwinda na mwendelezo wa ligi kuu kimeshuka dimbani leo kuikabili klabu ya Dodoma FC ambapo wekundu wa Msimbazi wameondoka na ushindi wa bao 1-0.

Bao pekee katika mchezo huo limefungwa na kiungo mshambuliaji Said Hamis Ndemla ambaye aliachia shuti kali akiwa katikati ya uwanja baada ya kupokea pasi kutoka kwa Jonas Mkude.

Simba ambayo inaongoza msimamo wa ligi kwa alama 11 itashuka dimbani Oktoba 14 kuvaana na Mtibwa Sugar kwenye mechi ya ligi kuu itakayopigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

More here:  

Timu ya Simba Kiboko…Mwendo wa Ushindi tu