Ndoa ya Zamaradi Yawaweka Kitimoto Antonio Nugaz na Adam Mchomvu

Ndoa ya Zamaradi Mtetema na mwanaume mmoja ambaye hakutambulika jina kale mara moja huku wengi wakidai ni ndugu wa kiongozi wa juu ya serikali ya awamu ya tano, imezua mtafaruku katika mitandao ya kijamii.

Mrembo huyo ambaye ni mama wa watoto wawili aliozaa na Mkurugenzi wa Vipindi vya Clouds Media, Ruge Mutahaba alifunga ndoa ‘kimyakimya’ mwisho wa wiki iliyopita.

Zamaradi alivunja ukimya kwa kuweka kwenye Instagram picha ya ndoa yake na mumewe ambaye hakuonekana vizuri sura na kuandika, “ALHAMDULILLAH!!”

Hata hivyo baada ya picha hizo kusambaa mitandaoni watu wengi walikuwa hawaamini kama ni kweli mrembo huyo ameolewa na mwanaume mwingine tofauti na bosi huyo wa Clouds Fm kutoka na wawili hao kuwa wasiri zaidi katika mahusiano yao.

Umma ulianza kuamini kwamba ni kweli mrembo huyo ameolewa na sio movie kama baadhi ya watu walivyokuwa wanafikiria baada ya watu wake wa karibu kumpost katika mitandao ya kijamii wakimpongeza kwa hatua waliyoifikia.

Mtangazaji wa Kipindi runinga cha Kambi Popote, Antonia Nugaz siku chache baada ya mrembo huyo kufunga ndoa alimpongeza mrembo huyo kwa kumtakia heri katika siku yake ya kuzaliwa ikiwa ni siku chache toka afunge ndoa.

“Moyo wako siku zote ndio kiashiria cha mitendo vyako, kheri ya siku ya kuzaliwa kwako allah Bariki, Zamaradi Mtetema,” Hii ni kauli ya Nugaz ambayo ilimfanya Adam Mchomvu kukomenti ujumbe ambayo ilionekana akimtuhumu Zama kumrekodi bosi wake Ruge.

Ujumbe wa Adam Mchomvu ambao aliutoa kupitia post ya Nugaz, iliibua maswali mengi mtandaoni huku mashabiki wengi wakiporomosha maneno ya kejeli huku vijembe vingi zikielekezwa kwa bosi huyo wa Clouds.

Bongo5 ilimtafuta Nugaz lakini mtangazaji huyo alitakaa kulizungumza sakata hilo kwa madai watalimaliza kiofisi.

Bongo5

This article:

Ndoa ya Zamaradi Yawaweka Kitimoto Antonio Nugaz na Adam Mchomvu