Mbunge CHADEMA Ataka Vyama Vingi Vifutwe

Mbunge CHADEMA Ataka Vyama Vingi Vifutwe

Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia CHADEMA John Heche, ameitaka serikali kufuta mfumo wa vyama vingi na kubakia na chama kimoja, kama wanaona uwepo wa vyama vya upinzani ni uhaini.

Akizungumza na moja ya Televisioni hapa nchini, John Heche amesema wamekuwa wakipokea vitisho vikali juu ya kufanya siasa na kukososa utendaji wa serikali, kitu ambacho ni wajibu wao kama vyama vya upinzani bungeni, hivyo kama wanaona wanafanya kosa basi ni heri wafute vyama hivyo.

John Heche ameendelea kusema kwamba kukosoa serikali sio uhaini bali ni kufanya kazi kadri ya sheria za nchi zinavyotaka, lakini kwa hali ya sasa hivi ilivyo imekuwa inaonekana kinyume, na kuhatarisha usalama wao na familia yao.

Continued: 

Mbunge CHADEMA Ataka Vyama Vingi Vifutwe