Manchester United, Man City Wavamia Italia

Timu za Manchester United na Manchester City zimeanzisha vita mpya ya kutaka kumsajili mchezaji wa Roma kutoka Italia, kiungo Lorenzo Pellegrini kwenye dirisha dogo la Januari.

Timu hizo zimejikuta zikigongana kwenye kumsajili mchezaji huyo ambaye dau lake limefikia Pauni 22 milioni kwa klabu yoyote inayotaka kumng’oa kikosini hapo.

Hata hivyo klabu ya Manchester United inaonekana kuwa mbele zaidi kwani imeshamfukuzia zaidi ya mara mbili na ikaamua kuachana naye, hata hivyo sasa imerudi tena kwa kasi huku wakigongana na watani zao Man City.

Credit:

Manchester United, Man City Wavamia Italia