Watu 15 wafariki kwenye ajali

Kamanda wa polisi mkoani Rukwa amethibitisha kuwa watu 15 wamefariki dunia na wengine 9 kujeruhiwa, baada ya lori lenye mizigo walilokuwa wakisafiria kupata ajali wilayani Nkasi mkoani humo.

Kamanda wa polisi mkoani Rukwa George Chando, amesema kuwa ajali hiyo imetokea kwenye tarafa ya Kate wilayani Nkasi, ikihusisha gari aina ya Fuso lenye nambari T425 BFF ambayo ni mali ya Bakari Kessy ambaye ni mtoto wa mbunge wa jimbo la Nkasi Ali Kessy.

Imeelezwa kuwa dereva wa lori hilo amekimbia baada ya ajali giyo, ambayo kwa taarifa za awali linasemakana kuwa limepata ajali kutokana na mwendo kasi na kwamba kati ya manusura 9, wanaume ni 6 na wanawake 9.

Fuso hiyo ilikuwa ikitokea kijijini Mvimwa kuelekea kijiji cha Wampembe, na sambamba na watu hao pia lilibeba magunia ya mahindi.

Kamanda wa polisi usalama wa barabarani nchini, amesema kuwa barabara iliyosababisha ajali ni mbovu ikiwa na makorongo, ambavyo mwendokasi wa dereva aliyekimbia usingemwezesha kupitisha gari hilo salama.

The post Watu 15 wafariki kwenye ajali appeared first on The Choice.

From: 

Watu 15 wafariki kwenye ajali