Tunafanya Haya Kutengeneza Tanzania Mpya- Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali ya Tanzania imenunua ndege sita ikiwepo ndege moja yenye uwezo wa kutoka Dar es salaam hadi Marekani moja kwa moja na ndege hizo zitakuja mwakani 2018, huku akiwataka watanzania kuunga mkono juhudi zake kwani anafanya hivyo kwa ajili ya kutengeneza Tanzania mpya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Magufuli

Rais Magufuli amesema hayo kwenye Mkutano wa 33 wa Jumuiya Ya Tawala za Mitaa (ALAT) ambao umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

“Tumenunua ndege sita ndege mbili zimeshawasili Tanzania, lakini ndege zingine ikiwepo Bombardier zitawasili mwakani 2018 mwanzoni. Tunafanya haya kwa ajili ya kutengeneza Tanzania mpya, nchi ambazo zina ndege zake idadi ya watalii wanaoingia kwenye nchi hiyo ni kubwa zaidi, nchi yetu ni ya pili kwa kuwa na vivutio vingi duniani lakini idadi ya watalii wanaoingia ni ndogo kutokana na kukosa ndege zetu”amesema Rais Magufuli.

Kwa upande mwingine Rais Magufuli amewaonya watumishi wa umma wakiwemo wakurugenzi wenye tabia za ulevi na kuwambia waache tabia hiyo mara moja kabla ya kuwatumbua.

Originally posted here:

Tunafanya Haya Kutengeneza Tanzania Mpya- Rais Magufuli