Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) Kutoa Msimamo wao Kauli ya Rais Magufuli

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), limesema linatarajia kutoa msimamo wao hivi karibuni kufuatia kauli ya Rais Magufuli ya kutoongeza mshahara, mara baada ya vikao vyao na serikali kufanyika.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Katibu Mkuu wa TUCTA, Yahya Msigwa amesema wanakusudia kuonana na uongozi wa serikali ili kujadili suala hilo, na ndipo watatoa msimamo wao kama hawatafikia makubaliano mazuri.

“Tunahitaji kuonana na uongozi wa serikali tujadili, kuna mambo mengi ya kujadili sio la mishahara tu, kwa muda mrefu vikao vimekuwa havikaliwi, hata vikikaliwa havina majibu, sasa hivi lazima tulitafutie ufumbuzi kwa sababu changamoto ni nyingi, wafanyakazi hawana hali nzuri kabisa, malalamiko ni mengi mno”, amesema Yahya Msigwa.

Hapo jana Rais Magufuli ametoa kauli ambayo imeibua sintofahamu nyingi kwa wananchi, baada ya kusema hajaongeza mishahara na hatoongoze mishahara kwa wafanyakazi kwa kipindi chote atakachokuwepo madarakani.

Link: 

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) Kutoa Msimamo wao Kauli ya Rais Magufuli