Nuh Mziwanda Aitamani Ndoa ya Mr. Blue na mkewe

Msanii wa bongo fleva Nuh Mziwanda ameibuka na kusema kwamba hana mpango wa kurudi nyuma na kurudiana na aliyekuwa mke wake Nawal kwa kuwa bado ana utoto mwingi, na kusema kwamba anayatamani maisha ya ndoa ya Msanii Mr. Blue na mkewe

kwani wanaheshimiana
Nuh amelazimika kusema maneno hayo baada ya kukubali kufunguka juu ya kuachana na mke wake ambaye pia ni mama wa mtoto wake na kusema kwamba mke wake huyo bado ana akili za kitoto sana na ndizo zilizompelekea kupiga picha na mwanaume mwingine na kudai amefunga ndoa kisha kuwatumia marafiki zake, kitu ambacho amedai mke wa Mr. Blue hana mambo hiyo
“Mimi naangalia sana maisha ya Mr. Blue na mke wake, Mke wa Byser hana michongo hii.

Wanaheshimiana lakini mimi na sijui nimemkosea wapi Nawal na kusema kama ningekuwa nimemkosea angeniambia hata chumbani. Nashangaa kwa nini tulidumu kwenye uchumba halafu kwenye ndoa ndiyo tusidumu. amesema

“Nawali bado ana utoto mwingi sana mpaka sasa hajaamua kuwa mke wa mtu na kumuheshimu mume wake kama mke ninachoamini ni kwamba mungu alimleta Nawal kwenye maisha yangu kwa ajili ya kuzaa naye mtoto na sio kuishi naye. Kama pia familia yake inaangalia matendo ya mtoto wao akienda kwenye media na kuzungumza vitu visivyokuwa na ukweli basi familia inakuwa siyo staha kwani ilipaswa wamshahuri vyovyote “aliongea Nuh.

Aidha Nuh ameongeza kuwa yeye kuamua kurudi kwenye dini yake aliamua kumpa sababu mke wake ya kuachana kwani alikuwa akihangaika kutafuta sababu kwa muda mrefu hadi kuchangia kutokuwa na amani.

“Mke wangu alikuwa akitafuta sababu za kuachana na ndiyo maana niliamuakurudi kwenye dini yangu. Yeye sasa hivi kusema hajaolewa ni ‘Too Late’ kwani siwezi kurudi nyuma. Mama yangu na muziki wangu ndiyo vinanifariji sana. Mke mwema nitaletewa ambaye nikimkosea ataniambia na tutavumiliana ili maisha yaendelee

Originally posted here¬†–¬†

Nuh Mziwanda Aitamani Ndoa ya Mr. Blue na mkewe