Naomba Ushauri: Mama Mkwe Amemtafutia Mke Wangu Mchepuko

Nina jamaa yangu mpaka hivi sasa dunia anaiona chungu na hajui achukue uamuzi gani dhidi ya mkewe na mkwewe

Jamaa ameoa mwanamke ambae tayari alishaolewa na kuzaa mtoto mmoja ila kutokana na maisha kuwa ya tabu mume aliondoka kuelekea mozambiq kuchimba madini na hakurudi tena mpaka jamaa yangu alipojitwisha majukumu ya kuoa

Tatizo linalomsumbua jamaa yangu ni pindi alipooa aliamua kwenda kuishi na mke wake nyumbani kwao lakini pale kwao ikatokea sintofahamu na dada wa jamaa yangu ikabidi waende wakapange chumba,kule mama mkwe ikawa kila asubuhi lazima aje ashinde pale home kwa gia ya kujifanya anacheza na wajukuu na jioni anabeba chakula

Kupita kama miezi sita tangu ule mchezo uanze mama mkwe akatoa ushauri kwanini wasihamie kule nyumbani yaani ukweni sababu nyumba ipo na nafasi na yeye mama mkwe atapunguza msafara wa kuja pale daily,jamaa yangu akashauriwa akakubali wakahamia ukweni sasa baada ya kuingia pale jamaa yangu ndio ameanziwa visa vya kuweza kuua mtu

Jamaa yangu yeye ni dereva wa daladala sasa siku moja alipata udhuru akarudi nyumbani akakuta mlango wa chumba chake umefungwa na mama mkwe yupo pale barazani anafanya shughuli zake jamaa kuuliza akaambiwa mke ametoka akapiga simu haikupokelewa jamaa akaondoka siku nyingine akarudi tena hali ni ile ile jamaa akamuuliza mama mkwe kwani mama zuberi akiondoka haachi funguo

Akajibiwa haachi basi jamaa jioni ikabidi angushe mtiti, kumbe pale kuna jirani anauona mchezo mzima ikabidi amg’ate sikio jamaa yangu ya kwamba kuna jamaa huwa anaingia pale na mama mkwe anawafungia kufuli kwa nje mpaka wanapomaliza shughuli zao na hawakuanza leo

inavyoonekana mkwe anampenda mwizi zaidi kuliko mkwe halali

Sasa mpaka muda huu jamaa amechanganyikiwa na mama mkwe amesema jamaa akitaka ahame yeye mwanawe abaki pale na mke ana mpenda na anafikiria watoto wake

Naomba tumsaidie ushauri maana ameathirika kisaikolojia

By Madala

Originally posted here:  

Naomba Ushauri: Mama Mkwe Amemtafutia Mke Wangu Mchepuko