Tume ya Uchaguzi Kenya Yaitisha Mkutano na Wagombea wa Urais

Tume ya Uchaguzi Kenya Yaitisha Mkutano na Wagombea wa Urais

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amefika kwenye mkutano ulioitishwa na tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC katika ukumbi wa Bomas of Kenya mjini Nairobi.
Rais Uhuru Kenyatta naye amealikwa kwenye mkutano huo na IEBC inatarajia kuwa atafika.

Tume ya IEBC ilitisha mkutano na wagombea hao wakuu wa urais kabla ya uchaguzi wa tarehe 26 mwezi huu, kujadiliana kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo.
IEBC imewaalika rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga, siku moja baada kufanya mazungumzo na wajumbe 12 kutoka nchi za kigeni wakiongzowa na balozi wa Marekania nchini Kenya Robert Godec na naibu balozi wa Uingerzea nchi Kenya,Susie Kitchens, ambao wamewataka wanasiasa kuheshimu uhuru wa tume ya uchaguzi.

Kufuatia kuporomoka kwa mazungumzo kati ya waakilshi wa chama cha Jubilee, chama cha National Super Alliance (NASA) na tunme ya IEBC siku ya Alhamisi, mwenyekiti wa tume ya IEBC Wafula Chebukati, alisema kuwa alitaka kukutana ana kwa ana na wagombea wakuu akiwalaumu waakilishi wao kwa misimamo mikali.
Wakiongea na waandishi wa habari siku ya Jumatatu wanadiplomasia hao waliitaka Jubilee na NASA kuacha kutumia maneno makali na kutochukua misimamo ambayo inahujuma shughuli ya upigaji kura.

See the original article here:

Tume ya Uchaguzi Kenya Yaitisha Mkutano na Wagombea wa Urais