Rais Magufuli ataja sababu ya kutumbua wakurugenzi 4 aliowateua

Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za mitaa Tanzania (ALAT) Rais Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa anazo taarifa za uwepo wa Wakurugenzi wanne wa Halmashauri ambao ni walevi na kusema kwamba, hao wajihesabu kwamba wameshaondoka.

Afunguzi huo umefanyika leo Dar es Salaam ambapo mkutano huo utafanyika kwa siku nne.

Ameonya viongozi kuhusu matumizi ya vilevi hasa muda wa kazi na kusema kuwa, miongoni mwa viongozi waliojitokeza katika mkutano huo kuwa, kama kuna yeyote ambaye ni mlevi, basi aache mara moja ili angalu aonekane amebadilika apone.

Mbali na hilo, Rais Magufuli amewaagiza viongozi hao wa serikali za mitaa kuhakikisha wanahimiza wananchi kujishughulisha na kilimo chenye tija ili waweze kupata chakula kwani serikali haitotoa chakula kwa watu wasiofanya kazi.

“Tuhamasishe watu kufanya kazi,Nilishasema sitatoa chakula cha Msaada kwa wilaya ambayo watu hawataki kufanya kazi.”

Source:  

Rais Magufuli ataja sababu ya kutumbua wakurugenzi 4 aliowateua