Mtandao wa WhatsApp wazindua emoji mpya

Mtandao wa WhatsApp Oktoba 2 mwaka huu umezindua emoji zake mpya baada ya kuwa wametumia zinazomilikiwa na Kampuni ya Apple kwa muda mrefu.

Kampuni hiyo tanzu ya Facebook ilizindua emoji hizo Jumatatu ambazo zitakuwa zikitumika katika mtandao huo.

Kwa kipindi cha nyuma WhatsApp imekuwa ikitumia emoji za Apple, si tu kwenye iPhone na Mac, lakini pia katika simu na vifaa vinavyotumia mfumo wa uendeshaji (OS) wa Android na Windows.

Licha ya WhatsApp kuzindua emoji hizo mpya, kwa kiasi kikubwa inaonekana zimefanana na ambazo Apple wanazitumia. Wakati mwingine ni vigumu kuonesha utofauti kati ya emoji za WhatsApp na Apple.

Hii haimaanishi kwamba haziwezi kutofautishwa, kwani ukiangalia kwa ukaribu namna zilivyowekwa, utaweza kubaini tofauti kati yao.

Mabadiliko haya kwa sasa yanaonekana kwa wale tu wanaotumia WhatsApp Beta na huenda kukawa na mabadiliko zaidi kabla hazijaanza kupatikana kwa watumiaji wote.

Read this article: 

Mtandao wa WhatsApp wazindua emoji mpya