Mimba ya Mwanafunzi Yamfikisha Mahakamani Mtendaji

Ofisa Mtendaji  Afikishwa Mahakamani Tuhu

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ihulike wilayani Bukombe, Lucas Maganga amefikishwa katika mahakama ya wilaya kwa tuhuma ya rushwa.

Akimsomea shtaka hilo mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Gabriel Kurwijila, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wa wilaya hiyo, Kelvin Murusuri alidai Maganga alitenda kosa hilo Julai kwa tarehe na nyakati tofauti.

Alidai kuwa baada ya mshtakiwa kupata taarifa za ujauzito wa mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Ihulike, alizikutanisha familia mbili za upande wa msichana na mvulana aliyempa ujauzito kisha akizishawishi zielewane.

Aliendelea kuiambia mahakama kuwa baada ya ushawishi huo, Stephano Maliyatabu ambaye ni mzazi wa mvulana alitoa Sh950,000, kati ya fedha hizo mtendaji alipewa Sh450,000 na nyingine alipewa mzazi wa msichana huyo. Hata hivyo, mshtakiwa alikana shtaka hilo na upande wa mashtaka ulidai uchunguzi umekamilika. Mshtakiwa alikosa wadhamini wawili waliopaswa kusaini dhamana ya Sh3 milioni kila mmoja na hivyo kukosa dhamana. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 12.

From¬†–¬†

Mimba ya Mwanafunzi Yamfikisha Mahakamani Mtendaji