Kijana wa Azam U-20 Apata Shavu Kuchezea Kikosi cha Kwanza cha Timu Hiyo

Kijana  wa Azam U-20 Apata Shavu  Kuchezea Kikosi cha Kwanza cha Timu Hiyo

Kocha mkuu wa Azam FC Aristica Cioaba amesema ataendelea kutoa nafasi kwa vijana watakaoonyesha uwezo wa kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari leo kocha huyo ameanza kwa kusifu kiwango kilichooneshwa na kinda wa timu ya vijana ya Azam FC (Azam U-20), Paul Peter kwenye mchezo dhidi ya Singida United uliopigwa wikiendi iliyopita.

“Paul (Peter) ni mshambuliaji mzuri kijana, licha ya uchanga wake haikunipa shida mimi kama kocha kuweza kumpa nafasi kwenye mechi iliyopita”, amesema Cioba.
Muromania huyo ameongeza kuwa kama alivyompa nafasi Paul Peter ataendelea kutoa nafasi kwa vijana wengine ambao wanaonesha uwezo wa kutoka timu za vijana za Azam FC.

Paul Peter alipandishwa kwenye kikosi hicho Jumanne iliyopita, nakutumia siku nne tu kufanya mazoezi na kikosi cha wakubwa kabla ya Jumamosi kufunga bao la kusawazisha na Azam FC kuvuna pointi moja dhidi ya Singida United kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

See the original article here:  

Kijana wa Azam U-20 Apata Shavu Kuchezea Kikosi cha Kwanza cha Timu Hiyo