Chege Amtaja Aslay Kama Msanii Bora wa Muda Wote

Msanii wa muziki Bongo, Chege amefunguka na kutaja ngoma zake anazozikubali, msanii anayeimba ambaye ni bora kwake kwa muda wote pamoja na rapper.

Chege ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Run Town’ ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa ngoma zake ambazo anazikubali kwa muda wote ni Karibu Kiume, Twenzetu na Uswazi Take Away.

Pia amemtaja msanii Aslay kuwa msanii wake bora wa muda wote pamoja na Marehemu Mangwea kuwa rapper bora wa muda wote.

Excerpt from: 

Chege Amtaja Aslay Kama Msanii Bora wa Muda Wote