Mwanamuziki Maua Sama Afunguka Kuhusu Kuolewa

WIKI chache baada ya kuchumbiwa na Mzungu, staa wa Muziki wa R&B, Maua Sama amefunguka kuwa ataolewa mwakani.

Akichonga na Over Ze Weekend, Maua alisema kuwa kila kitu kinakwenda kwa utaratibu wake na kwamba suala la ndoa huenda likawepo mwakani na siyo mwaka huu.

“Bado sana mipango ya ndoa labda mwakani. Sasa hivi naangalia muziki zaidi na nashukuru nimeweza kukaa kwa muda mrefu bila kuchuja na hii ni kutokana na msanii unavyojiweka,” alisema Maua.

Imelda Mtema | Ijumaa Wikienda

View original post here: 

Mwanamuziki Maua Sama Afunguka Kuhusu Kuolewa