Msanii wa Bongo Fleva Ochu Akiri Kuwa Mume Bwege Mbele ya Witness

Msanii Ochu Shegy ambaye ni mpenzi wa msanii Witness anayefanya muziki aina ya Hip hop, amekiri ni kweli huwa anakula magengeni badala ya nyumbani kama ambavvyo inatakiwa kwa mwanaume ambaye anaishi na mke ndani.

Akizungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV, Ochu Sheggy amesema ni kweli anakula chips za magengeni kama Witness hajapika, kwani muda mwingine anakuwa amechoka hivyo hawezi kumlazimisha kumpikia.

“Huwezi ukatoka na mwanamke ye anafanya muziki we unafanya muziki, muda mwengine mnakuwa na ‘studio session’ mnarudi nyumbani saa 7 usiku, unamuingizaje jikoni mtoto wa watu? Kachoka tunaenda kutafuta chakula tule wote, sio robot yule”, amesema Ochu.

Ochu Shegy ameendelea kwa kumtetea mpenzi wake huyo ambaye inasemekana anampelekesha kutokana na ubabe wake, na kusema kwamba Witness sio mbabe na hawezi kumfanyia ubabe, kwani iwapo angekuwa anafanya hivyo, angeshaondoka na kwenda kwa wengine.

“Nahisi napendwa zaidi, mimi sio mtu ambaye naweza nikatulia sehemu jambo likiwa limeniumiza, naosha dakika sIfuri tu kwa sababu kuna bebes kibao, kwa nini ung’ang’anie sehemu unayoteseka? Siteseki, nafurahia”, amesema Ochu Sheggy.

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi za wawili hao kuachana, lakini Ochu alikanusha tetesi hizo kuwa hazina ukweli wowote, kwani bado wanapendana sana.

Read article here¬†–¬†

Msanii wa Bongo Fleva Ochu Akiri Kuwa Mume Bwege Mbele ya Witness