Maskini..Mtoto Aungua Moto Akiwa Amelala

Mtoto wa miaka miwili wa kike aliyefahamika kwa jina la Brightness Barnabas amefariki dunia akiwa amelala ndani ya nyumba baada ya nyumba kuungua moto kutokana na hitilafu ya umeme mkoani Shinyanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema chanzo cha moto huo ilikuwa ni hitilafu ya umeme.

“Nyumba ya Barnabas Saimoni (35) ambaye ni Msukuma anajishughulisha na kilimo mkazi wa kijiji cha Kakolo iliungua moto na kusababisha kifo cha mtoto binti aitwaye Brightness Barnabas mwenye umri wa miaka miwili” alisema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule.

Originally from: 

Maskini..Mtoto Aungua Moto Akiwa Amelala