Manara Awatupia Lawama Waamuzi wa Mchezo wa Jana Asema ‘Awakawii Kunifungia’

Manara Awatupia Lawama Waamuzi wa Mchezo wa Jana Asema 'Awakawii Kunifungia

Afisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara amefunguka na kuwarushia lawama waamuzi wa mchezo wa uliyochezwa jana kati ya Stand United dhidi ya Simba SC kuwa walichokifanya siyo sahihi kwa kulikataa goli la wazi na kisha kutoa penati yenye utata.

Manara amesema hayo kupitia ukurasa wake maalum wa instagram baada ya kumalizika mchezo huo ambao Simba walitoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-1 na hatimaye kuweza kupata alama tatu za mchezo huo.
“Hii ndiyo ligi ya Bongo na hao ndiyo marefa wetu. Unatoa penati tata kisha unakataa goli halali, fowadi anamkimbia beki unasema kaotea!. Acha nipige kimya hawakawii kunitia ‘lock up”, amesema Manara.
Simba SC kwa sasa inashikilia usukani wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa alama 11 ikifuatiwa na Mtibwa Sugar pamoja na Azam FC kwa alama hiyo huku wakitofautiana idadi ya magoli ya kufungwa na kufunga.

Link¬†–¬†

Manara Awatupia Lawama Waamuzi wa Mchezo wa Jana Asema ‘Awakawii Kunifungia’