Biashara ya Kununua Madiwani Hata Iringa ilifanyika – Mhe. Peter Msigwa

Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa amesema jimboni kwake pia biashara ya wabunge wa Chadema kununualiwa na CCM ilifanyika hivyo Mkurugenzi wa TAKUKURU, Valentino Mlowola kufungua jalada.

Akizungumza nae leo nje ya Ofisi za TAKUKURU, Mhe. Msigwa alieongozana na Wabunge Nassari na Lema kuingia katika ofisi hizo amesema wahusika wakuu ni RC na DC na baadhi ya polisi wanahusika na biashara hiyo.

“Kwa kifupi iringa mjini nako biashara ya kununua madiwani ilifanyika na nina ujasiri mkubwa mhusika mkuu ilifanyika na nina uhakika biashara ya kuwa nunua madiwani Iringa mjini ni ofisi ya RC pamoja na DC na baadhi ya mapolisi kwahiyo hii ilikuwa ni episode mliona ya Arusha vilitumika vifaa vyua Uingereza lakini kwetu sisi tulitumia vifaa vya Australia na sisi tutafungua jalada kama Mkurugenzi wa TAKUKURU alivyotushauri,” amesema Msigwa.

“Kwahiyo tusubiri kwasababu tumekabidhi kwenye korido za serikali na tunataka sheria ichukue mkondo wake ili uongo uongo wa kusema kuna watu wanmaunga mkono utendaji tunataka ufike mwisho ili watu wakae kwenye nafasi zao kwa haki na jinsi watu walivyopamua kuwa na kuwa chagua kwa kifupi ndo hivyo.”

Link – 

Biashara ya Kununua Madiwani Hata Iringa ilifanyika – Mhe. Peter Msigwa