Witness Awabwatukia Wasichana Wanaojiona Wazuri Mjini Adai Wanatembeza Sehemu za Siri ila Kuolewa Ng’oo

Msanii ambaye ni Raper wa kike kwenye game ya bongofleva, Witness, amewajia juu watu ambao huwatoa kasoro wenzao mitandaoni hususan wanawake, huku akionesha kushangazwa na wao kutopata ndoa kwa uzuri walionao

Kwenye ukurasa wake wa instagram Witnes ameandika ujumbe akisema kuwa watu wanaofanya hivyo hawana hofu ya Mungu aliyeymba, lakini kinachoshangaza wao wanaojiona wazuri wanaishia kuchezewa na wanaume bila kuolewa, kwa sababu hakuna mwanaume anataka mwanamke mwenye hulka zao.

“Huwa wananikera sana watu wanaofata fata mambo ya wenzao na kuwasema kuwa ni wabaya na wana sura nzito cha ajabu ni kwamba yeye ana msema mwenzie ya kuwa mbaya na ana sura nzito kaolewa, nyie wakati mmebaki tu insta mnabung’aa na kutembeza sehemu za siri kwa wame za watu tu, kama wazuri sana si mngeolewa sasa? mbona mnapuyanga tu na kudanga danga? Kwa tabia za kujiona wazuri sana ndo maana wengi mnaishia kumegwa tu mnaachwa”, ameandika Witness

Pia Witness ameendelea kwa kuwapa somo watu hao akiandika…

“Hakuna mwanaume anataka mwanamke machepele mfuatilia mambo ya watu mgonga hodi majumbani mwa watu kwako hutulii kutwa kushinda salon. Na wengine huwa mnanikera kama hamtozaa, je hao mnao wasema wanasura ngumu wangekua watoto wenu mngejisikiaje usikie mtu anawaambia hivyo? utapenda kweli? Hebu shikweni na aibu ya uzazi na mumuogope mwenyez Mungu! ameandika Witness kwenye ukurasa wake wa instagram.

Msanii Witness hivi karibuni amekuwa akipokea matusi kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuweka picha za nusu utupu, kitendo ambacho kimeonekana sio kizuri kwa jamii

Visit link:

Witness Awabwatukia Wasichana Wanaojiona Wazuri Mjini Adai Wanatembeza Sehemu za Siri ila Kuolewa Ng’oo