VIDEO-Nassari Aweka Hadharani Jinsi Madiwani Walivyorubuniwa Arusha

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari ameweka hadharani ushahidi wa rushwa na waliopewa madiwani ambao wamejiuzulu Chadema.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili, Nassari ambaye ameambatana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema walitoa ushahidi huo na kueleza wataukabidhi Takukuru na katika taasisi nyingine.

Katika ushahidi huo viongozi kadhaa wamerekodiwa wakiwashawishi madiwani kuhama na baadhi waliahidiwa wangelipwa posho za vikao vyao vilivyobaki hadi 2020 na kukamilishwa miradi yao.

Miongoni mwa makubaliano hayo ni kuwa wapewe fedha na kupata ajira na kukamilishwa miradi yote ya maendeleo waliyoahidi.

Wakati Nassari akifanya hivyo tayari baadhi ya madiwani waliojiuzulu walisema kuwa hawakushawishiwa na mtu yeyote wala kupewa rushwa bali wamehama kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli.

Link to original: 

VIDEO-Nassari Aweka Hadharani Jinsi Madiwani Walivyorubuniwa Arusha