Mwanaume Usione Aibu Kutongoza, ni Sehemu ya Kutimiza Wajibu Wako

Kuna hii tabia ya vijana wa kiume kuogopa kutongoza hasa kwa kuhofia kua watakataliwa. Kwanza ni kosa kuhofu au kua na mawazo ya kukataliwa au kushindwa katika maisha.

Jambo la pili na kubwa zaidi ni kwamba kutongoza ni sehemu ya kutimiza majukumu yako kama mwanaume. Huna haja ya kuhofu kutimiza majukumu yako hata kama utakosea.

Ukizaliwa tu mwanaume, kutongoza ni sehemu ya majukumu yako makuu kwenye Job Discription(JD) yako.

Tongoza kila mwanamke unaedhani au kuona unaweza kutongoza, tongoza kadri uwezavyo au upendavyo, usihofu kukataliwa, hofu kutokutongoza ila sio kukataliwa. Jisikie mwenye hatia kutokutimiza wajibu wako kuliko kujisikia hofu ya kukataliwa katika kutimiza wajibu wako.

Jifunze hata kwa ndege na wanyama, jogoo hutongoza kila tetea anaemuona bila kujali atafanikiwa au la, akifanikiwa hewala, akikosa alikua anafanya mazoezi ya kukimbia na kuweka mwili sawa.

Lakini pia usiogope kutongoza mwanamke mzuri kwa kuhofu kua lazima atakua na mume/mpenzi, wewe tongoza, sio kila mwanamke mzuri basi ana mume, wengi hua ni vacancy, ukijaribu unaweza kufill hiyo nafasi. Tongoza mahala popote u apojisikia au kuona kuna mtu unaweza kumtongoza na muda wowote.

Ni ushauri tu na kukumbushana.

Excerpt from: 

Mwanaume Usione Aibu Kutongoza, ni Sehemu ya Kutimiza Wajibu Wako