Mambo muhimu yatakayodumisha penzi lako

Wakati unampata mpenzi wako uliye naye akili yako ilikuwa inawaza mambo ya furaha na kila mmoja alijitahidi kumfanya mwenzake kuwa mwenye furaha.

Hiyo ndiyo furaha kubwa katika mapenzi, kuwa na furaha na maelewano baina ya wewe na mwenza wako. Lakini je, umewahi kuwaza kuwa kuna nyakati zitafika wewe na wenza wako mtagombana?  kama hukuwa umewaza hivyo basi tambua kuna wakati utafika kwani hakuna binadamu aliyekamilika.

Lakini hilo lisikutie shaka, ni sehemu tu ya maisha ya mapenzi yanayohitaji uvumilivu.

Ukweli ni kwamba, pamoja na kwamba kuingia katika mahusiano ni jambo la furaha lakini inahitajika nguvu kubwa na kujitoa kwingi ili lidumu. Siyo hivyo tu, bali wewe na mwenza wako mnapaswa kufanana.

Ndiyo. Kufanana. Siyo kufanaan kwa sura, hapa inabidi muwe na mambo ya kufanana, muwaze vya kufanana na mfanye mambo ya kufanana. Hapa unaweza ukajiuliza mtu utawezaje kufanana na mwenzi wako wakati kila mmoja ana tabia yake?

Jambo la msingi ni wewe na mwenza wako kukubali kuachia baadhi ya mambo ambayo mnahisi siyo ya faida katika mapenzi yenu. Si vyema kung’ang’ania jambo wakati halimfurahishi mwenza wako na wakati huo huo siyo la muhimu.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo wewe na mwenza wako mnapaswa kufanana (things you must have in common) ili mapenzi yenu yadumu;

Malengo

Unapotaka kuingia au unapokuwa katika mahusiano, lazima wote wawili muwe na matarajio. Inabidi muweke malengo na mipango ya naisha yenu. Nini lengo la ninyi kuwa wapenzi, Siyo mnakuwa tu katika mahusiano alimradi uonekane kuwa una mpenzi.

Urafiki

Kuwa rafiki na mpenzi wako ni jambo la muhimu sana katika kudumisha uhusiano wenu. Wapo watu watakaojiuliza kuwa unakuwaje na mpenzi halafu siyo rafiki yako. hiyo inawezekana kabisa na huwa inawatokea wengi, yamkini hata wewe una mpenzi asiye rafiki yako.

Tunaposema urafiki katika mapenzi, ni ile hali ambayo unakuwa muwazi kwa mwenza wako, unataniana nae, uko tayari kumueleza matatizo yako, unamumini na nde unayemtafuta wa kwanza pale unapopatwa na msongo wa mawazo au tatizo lingine lolote. Wapo watu ambao hawawezi kujadiliana na wapenzi wao baadhi ya mambo, badala yake huwatafuta marafiki zao wa karibu na kuwashirikisha. Ili penzi lako liwe lenye afya na lililonawiri, inakupasa ujenge urafiki baina yako na mwenza wako.

Heshima

Moja ya mambo yanayofanya penzi lidumu ni pamoja na heshima. Mambo unayotakiwa kujiuliza ni je, mpenzi wako anakuheshimu? wewe unamuheshimu? anaongea na wewe kwa heshima? yuko tayari kuyaheshimu mawazo yako hata kama hayamfurahishi? na mengine mengi. Kufanya hivi kutawafanya wote kujiona mnathaminiana na kutaliimarisha penzi lenu na hakika mtafurahia uhusiano wenu.

Kuaminiana

Kuaminiana ni nguzo kubwa ya kudumisha upendo baina ya wapenzi. Hakuna jambo la hatari kama kuwa kwenye mahusiano na mtu usiyemuamini. hilo litakufanya kuishi kwa wasiwasi na hata kuanza kuwaza yasiyo mema juu ya mwenzi wako.

See original article here: 

Mambo muhimu yatakayodumisha penzi lako