CHADEMA yataka Bei ya Ukumbi Ikulu ili Wengine Nao Wakiwa na vikao vyao Wasisite Kwenda

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeitaka Serikali kuweka wazi utaratibu unaosemwa kwamba ulifuatwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), kufanya mkutano wao wa Chama Ikulu jijini Dar es salaam, ili kila mmoja ajue iwapo atahitaji kwenda kufanya mkutano hapo.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bwana John Mrema, amesema kama ukumbi huo wa Ikulu unaruhusiwa kifanyika mkutano na mtu yeyote, basi waweke wazi utaratibu wa bei ili wengine nao wakiwa na vikao vyao wasisite kwenda ili kuongeza pato la Taifa.

Chanzo: East Africa Television

Originally posted here:  

CHADEMA yataka Bei ya Ukumbi Ikulu ili Wengine Nao Wakiwa na vikao vyao Wasisite Kwenda