Nimemkuta Mpenzi Wangu na vitu Nisivyovielewa, Naomba Msaaada Wenu Kuvielewa

Nipo na mpenzi Wangu ambaye ninaamini ndie nampenda kuliko wanawake wote na ninamatarajio ya kufunga naye ndoa. Mara kwa mara huwa anakuja kulala kwangu hata Siku 2 na kurudi kwao.

Juzi aliponitembelea na kuingia bafuni nikashawishika kuchungulia ndani ya kipochi chake. Nikashituka baada ya kukuta vitu viwili.

1. Kikaratasi chenye unga wenye chembechembe ambazo zinaonekana ni mizizi iliyotwangwa kikiwa kimeandikwa “kuchoma”.

2. Hiki kingine ambacho sijakitambua ni vijiti viwili. Kirefu na kifupi vikiwa vimeunganishwa na kamba. Kwa anayejua kuhusu hivi vijiti anisaidie uelewa.

Continued: 

Nimemkuta Mpenzi Wangu na vitu Nisivyovielewa, Naomba Msaaada Wenu Kuvielewa