JE Wajua Kuwa ni Watu Wawili tu Duniani Ndio Kamwe Hutaweza Kuwa’Bloku’ Facebook…?

Mmiliki wa Facebook Mark Zuckerberg na mkewe Priscilla Chan ndio watu pekee ambao huwezi kuwablock katika mtandao maarufu wa kijamii wa Facebook.

Mwanzoni kabla ya Mark Zuckerberg kumuoa Priscilla ni yeye pekee ndiye ambaye hakukuwa na uwezekano wa Kumbloku. Mark huandika taarifa nyingi kuhusu maboresho ya Facebook na taarifa mbalimbali kuhusu maisha yake binafsi au mambo mengine ya kijamii.

Kublock mtu ni njia mojawapo ya kutotaka aone posti zako wala zake. Njia hii unaweza kufanya asiwe rafiki yako (Unfriend) au kukufuata (Unfollow).

Ni kwamba unaweza kumblock mtu yeyote facebook kasoro yeye na mkewe tu! Ukiingia kwenye ukurasa wake option ya kumbloku ipo lakini haifanyi kazi. Ukibonyeza “block” inakuambia Block error.

Mark Zuckerberg na Priscilla Chan walikutana mwaka 2003 wote wawili wakiwa wanafunzi chuo kikuu cha Havard, na mwaka 2012 walioana baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa kipindi kirefu.

Kwa mujibu wa ripoti ndani ya The Independent, machapisho yote (ndani ya facebook) huonekana katika mifumo ya malekezo ya kitarakimu ya Facebook inayofahamika kama ‘algorithm’ na mwishowe kuzipeleka kwa wachangiaji mbalimbali.

Hivyo kumzuia mwasisi wa Facebook na mkewe kulikuwa ndiyo njia mwafaka ya kuepuka machapisho yanayorushwa kwenye kurasa za mtandao huo kuonekana kabla ya kupigwa kabisa marufuku. Zuio (Block) hilo limekuwapo tangu mwaka 2010

Kama utapenda kujaribu kumbloku Mark Zuckerberg na mkewe Priscilla Chan ingia katika kurasa zao unajaribu uone kama utaweza. Je huu si udikteta flani hivi?

Teknokona

Original article:

JE Wajua Kuwa ni Watu Wawili tu Duniani Ndio Kamwe Hutaweza Kuwa’Bloku’ Facebook…?