MKE wa Mzee Yusufu, Leyla Rashidi Azimia Nusu Saa Msiba wa Mke Mwenza…

MSIBA UNAUMA! Ndiyo maneno pekee unayoweza kusema baada ya mtandao huu kushuhudia mke mkubwa wa Mzee Yusufu, Leyla Rashidi akizimia katika msiba wa aliyekuwa mke mdogo wa mumewe huyo, Chiku Khamisi.

Leyla ambaye alifariki katika Hospitali ya Amana, jijini Dar siku ya Jumamosi na kichanga tumboni alipokuwa akijifungua, kumeibua simanzi nzito kwa watu kiasi cha kumpelekea mke mwenza, Leyla kupoteza fahamu kwa muda wa nusu saa msibani.

Mzee Yusuf akiwa na mwili wa kichanga kilichofariki pamoja na mama yake.
Watu waliokusanyika msibani hapo walishikwa na majonzi zaidi baada ya kumuona ‘Malkia’ huyo akipoteza fahamu kitu kilichoonyesha kuumizwa mno na msiba huo.

Chiku enzi za uhai wake.
Marehemu Chiku alizikwa jana (Jumapili) katika Makaburi ya Kisutu, jijini Dar. Mungu amlaze mahali pema peponi Bi Chiku, Amen.

GPL

View original post here – 

MKE wa Mzee Yusufu, Leyla Rashidi Azimia Nusu Saa Msiba wa Mke Mwenza…