Huddah Monroe aeleza sababu ya kuitosa Wasafi Beach Party

Wasafi Beach Party iliyofanyika Disemba 24, Jangwani Sea Breezy jijini Dar es Salaam, ilikuwa iwakutanishe mahasimu warembo Huddah Monroe na Vera Sidika jukwaani kama mahost.

Wengi tulikuwa tukisubiri kushuhudia drama ya kufungia mwaka kutoka kwa warembo hao wa Kenya, lakini bahati mbaya fahari mmoja hakutokea. Huddah Monroe ametumia Snapchat kuelezea sababu iliyomfanya ashindwe kuja kwenye party hiyo kuwa ni kushindwa kufikia makubaliano waliyokuwa wamejipangia na Diamond na hivyo ikamlazimu kukatisha kuja katika dakika za mwisho.

Hata hivyo Vera na mrembo mwingine wa Uganda, Anita Fabiola walikuwepo na kila kitu kilienda freshhh…

The post Huddah Monroe aeleza sababu ya kuitosa Wasafi Beach Party appeared first on The Choice.

Read the article – 

Huddah Monroe aeleza sababu ya kuitosa Wasafi Beach Party