VIDEO: Abiria watwangana ndani ya basi la Mwendokasi Dar

abiria watwangana ndani ya mwendokasi DAR

Kuna msemo unaosema Uzee mwisho Chalinze, msemo uliovuma sana kipindi cha nyuma hata hivyo msemo huo umeweza kujitokeza tena mchana wa jana 23 Desemba baada ya kutokea tafrani ndani ya basi la Mwendokasi (UDART) kwa wazee wawili kupishana kauli na kisha kuamua kushikana mashati.

Tukio hilo la aina yake, lilinzia kituo cha Magomeni Morocco ambapo abiria hao waliopandia basi lao hilo katika kituo hicho cha Magomeni kwa mmoja wapo kumkanyaga mwenzie na hali ikabadilika ghafla na kuanza kushikana mashati na kupigana

Wazee hao kila mmoja aliwa akimtambia mwenzie “Mimi huniwezi mtu wa mjini nimesoma mjini Azania Boys!” na Mzee Mwingine akajibu mapigo kuwa naye ni mtu wa mjini na amesoma mjini Tambaza Boys”.

Wazee ambao ni abiria na kila mmoja hakiwa na munkali, waliamua kuvaana na kuanza kupigana makonde hadi abiria wengie walipowaamulia.

Tazama video kuona tukio hilo hapa:

udart

Hapa Mzee mwenye miwani akionekana kwa pembeni akimvuta mkono Mzee mwenzake kabla ya kupandwa na hasira (mwenye shati la twiga cement)

dsc_0145

Hapa ngumi zilianza kwa wazee hao na kuamuliwa

Hapa waliamuliwa mwenye shati nyeupe akimsii Mzee mwenzake kuyaacha mambo hayo ya kupigana huku Mzee mwingine akizibitiwa na kijana mwenye tshit nyeupe kama anavyoonekana hapo pichani.

Hata hivyo Wazee hao waligeuka kuwa simulizi baada ya kumaliza ugomvi wao huo ambapo kila mmoja alikuwa akitamba namna alivyokuwa kijana ambapo mmoja alijisifia kuwa yeye alikuwa mtanashati na mstaarabu sio kama mwenzake  ambapo mwingine alisema yeye ni mstaarabu tokea wakati anasoma hivyo amekuwa na kuwa Mzee na ustaarabu wake.

The post VIDEO: Abiria watwangana ndani ya basi la Mwendokasi Dar appeared first on The Choice.

See original article here:  

VIDEO: Abiria watwangana ndani ya basi la Mwendokasi Dar