Hali ya barabarani leo ikionyesha msafara wa Wachaga kurejea makwao

moshi

Watu wengi sana hupenda kujumuika na ndugu, jamaa na marafiki katika msimu huu wa sikukuu wakisherehekea kwa pamoja baada ya mihangaiko ya mwaka mzima. Watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi husafiri kwenda maeneo mengine kwa ajili hiyo.

Licha ya kuwa watu wengi husafiri kurejea makwao lakini Kabila la Wachaga ndio waliojizolea sifa hii kubwa ya kupenda kurudi nyumbani kipindi hiki cha sikukuu huku wengine wakiwatania kuwa wanakwenda kuhesabiwa.

Ikiwa imebaki siku moja kabla ya sikukuu ya Krismasi, wakazi wengi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani leo walikuwa wakisafiri kuelekea mikoa ya Kanda ya Kaskazini mwa Tanzania. Lakini katika msafara huo, wengi wanaaminika kuwa ni Wachaga. Hapa chini ni picha za hali ilivyokuwa barabarani leo na kwenye moja ya hoteli ambapo abiria hupumzika na kupata chakula.

whatsapp-image-2016-12-23-at-9-37-31-pm-1whatsapp-image-2016-12-23-at-9-37-31-pm whatsapp-image-2016-12-23-at-9-46-27-pm-1

The post Hali ya barabarani leo ikionyesha msafara wa Wachaga kurejea makwao appeared first on The Choice.

Continue at source: 

Hali ya barabarani leo ikionyesha msafara wa Wachaga kurejea makwao